Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makame atoweka Kagera Sugar

Makame Yanga Def Makame atoweka Kagera Sugar

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka ndani ya kikosi cha Kagera Sugar zimethibitisha kuwa kiungo wao Abdulaziz Makame 'Bui' hajaonekana kambini kwa muda wa miezi miwili sasa na hakuna taarifa yoyote rasmi za wapi alipo mchezaji huyo.

Imefahamika kuwa, viongozi wa Kagera Sugar walimpa ruhusa ya muda mfupi kwa ajili ya matibabu lakini toka alipoondoka hajarejea na hakuna mawasiliano baina yake na klabu.

Taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Kagera Sugar zimethibitisha kuwa, uongozi umeamua kusitisha mshahara wa Makame kuanzia mwezi huu baada ya kukosekana mawasiliano baina ya uongozi na mchezaji huyo kutoka Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live