Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makame aonesha uungwana kwa Kapombe

Makame Abdulaziz Makame

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pengine labda ilikua ni presha ya mchezo baada ya kutulia, kukaa na kutafakari mchezaji wa Namungo FC, Abdulaziz Makame amemuomba radhi beki wa Simba SC, Shomari Kapombe na Watanzania husuani wapenda soka kwa ujumla.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Makame amemwomba radhi Kapombe kwa kumchezea mchezo usio wa kiungwana katika dakika ya 50, uliomfanya mwamuzi, Mwichui kumtoa nje kwa kadi nyekundu, hivyo kuigharimu timu yake kwa kubaki pungufu uwanjani na hatimaye kufungwa bao 1-0 kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa juzi.

Makame amesema haikuwa dhamira yake kucheza rafu hiyo bali lengo lake lilikuwa kutekeleza majukumu yake uwanjani kama mchezaji.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba radhi Watanzania na wapenda soka wote, kipekee zaidi nimwombe radhi mchezaji wa Simba, Shomari Kapombe kwa mchezo ambao sio wakiungwana, haikuwa dhamira yangu kumchezea rafu ni katika kutimiza wajibu wangu uwanjani kama mchezaji.

"Mpira ni mchezo wa amani na tunashauriwa kucheza 'Fair', timu yangu ya Namungo chini ya kocha wangu, Morocco [Hemed] naomba radhi kwa kuigharimu timu yangu kucheza pungufu. Naahidi kuzidisha umakini katika mechi zinazofuata," aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live