Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makame ajipanga upya kurudisha namba yake Yanga

95326 Pic+makame Makame ajipanga upya kurudisha namba yake Yanga

Tue, 11 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Kiungo wa Yanga, Abdul-Aziz Makame amepoteza namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, ila hilo kwake ni changamoto yakuboresha kiwango chake. Makame alisema anapambana kuhakikisha anakuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza, akiamini hicho ndicho kitakachomuonyesha kiwango chake kinapanda au la. Amesisitiza haogopi ushindani kwa wachezaji wanaopata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza, badala yake inamfanya kuwa makini siku akiaminiwa. "Ili timu iwe bora lazima kila nafasi iwe na ushindani, hii ni funzo kwangu kuendelea kujituma na kuhakikisha napata nafasi yakucheza mara kwa mara kwani ndicho kilichonileta Yanga," "Yanga ni klabu kubwa ina wachezaji wa kila aina kwa maana ya wageni na wazawa ambao wana uzoefu, bila kukaza buti inakuwa ngumu kuonekana ndio maana nasema nitacheza, kwani kinachotakiwa ni bidii," alisema Makame. Yanga imemsajili Makame akitokea Zanzibar katika timu ya Mafunzo, alipata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza chini ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera.

Chanzo: mwananchi.co.tz