Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makambo akabidhiwa Rungu la kuimaliza KMC

Heritier Makambo , Ebeneza Makambo ameanza mchezo wa leo

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Nabi, Naseddine Nabi amemuanzisha mshambuliaji Heritier Makambo katika eneo la ushambuliaji kwenye mchezo dhidi ya KMC.

Yanga na KMC zinashuka uwanjani leo saa 1:00 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kuanza kwa Makambo kumetokana na mshambuliaji Fiston Mayele kukosekana kabisa katika mchezo huo.

Kwenye mechi hii Nabi amefanya mabadiliko ya wachezaji baada ya kuwapumzisha kabisa Djuma Shaban, Khalid Aucho na Joyce Lomalisa ambao hata benchi hawapo na nafasi yao walianza Dickson Job na Farid Mussa.

Job aliwahi kucheza eneo la beki wa kulia katika mechi kadhaa msimu uliopita sambamba na Farid Mussa katika eneo la beki wa kushoto na bado wakatanya vizuri.

Kitendo cha Job kucheza kama beki wa kulia kumempa fursa Ibrahim Bacca kuanza na Bakari Mwamnyeto kwenye eneo la beki wa kati.

Upande wa KMC wao kikosi chao hakina mabadiliko na mchezo wao uliopita.

Vikosi vinavyoanza

Yanga: Djigui Diarra, Dickson Job, Farid Mussa, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Yanick Bangala, Gael Bigirimana, Tuisila Kisinda, Heritier Makambo, Stephen Aziz Ki na Dickson Ambundo.

KMC: David Kissu, Kelvin Kijiri, Hance Masoud, Andrew Vicent, Ibrahim Ame, Baraka Majogoro, George Makang’a, Styve Nzigamasabo, Matheo Anthony, Emmanuel Mvuyekure na Awesu Awesu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live