Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makambo Jr atimkia Ujerumani, alamba mkataba wa miaka 3

Makambo S.jpeg Athuman Masumbuko ‘Makambo Jr’.

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mshambuliaji wa Mashujaa FC, Athuman Masumbuko ‘Makambo Jr’ amejiunga rasmi na Klabu ya FCA Darmstadt ya Ujerumani kwa mkataba wa miaka mitatu.

Nyota huyo awali ilielezwa amemalizana na Coastal Union ili kuitumikia msimu ujao wa mashindano  ikiwemo Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika, japo baada ya kupata dili hilo akaamua kutua Ujerumani.

Akizungumza baada ya kukamilisha dili hilo, Makambo alisema, ni furaha kubwa kwake kuanza changamoto mpya huku akiweka wazi atahakikisha anapambana kwa ajili ya kuitangaza nchi kimataifa kama ambavyo wamekuwa wanafanya wachezaji wengine.

Kwa upande wa kocha Awadh Juma ‘Maniche’ aliyemfundisha akiwa na timu ya vijana ya Mtibwa Sugar U20 alisema, ni fursa nzuri kwa nyota huyo kuzidi kujitangaza kimataifa kwani kabla ya hapo alimtabiria kufika mbali zaidi kutokana na uwezo wake.

“Mchezaji anapopata nafasi ya kutoka nje ya mipaka ya Tanzania ni jambo la kushukuru kwa sababu anazidi kupata uzoefu wa kucheza na wachezaji mbalimbali, ni kijana mdogo mwenye malengo makubwa hivyo tumuombee kwa niaba ya taifa,” alisema.

Nyota huyo alijiunga na Mashujaa msimu uliopita wa 2023/2024 baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiichezea timu ya vijana ya Mtibwa Sugar iliyobeba ubingwa, huku akiibuka pia mfungaji bora kwa kutupia kambani mabao saba akiwa na kikosi hicho cha Umri chini ya miaka 20 (Mtibwa U20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live