Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makambo Ataja Siku Atakayofunga

Makambo Heritier Hat Trick Makambo Ataja Siku Atakayofunga

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HERITIER Makambo, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa ipo siku atafunga kwenye ligi kwa kuwa ni suala la muda hana mashaka nalo.

Kwenye ligi Yanga ikiwa imefunga mabao 22 katika mechi 12 ambazo imecheza, nyota huyo raia wa DR Congo hajafanikiwa kufunga wala kutoa pasi ya bao.

Makambo alisema kuwa anatambua kwamba mashabiki wanapenda kuona akifunga ila muda bado haujafika.

“Mashabiki wanapenda kuona nafunga hata mimi pia ninapenda kufanya hivyo lakini ni suala la kusubiri kwani bado kuna mechi za kucheza na mechi zipo nyingi hivyo ipo siku nitafunga,” alisema.

Nyota huyo amecheza mechi 10 kati ya 12 na kuyeyusha dakika 279 kwenye mechi za ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live