Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makaka arejesha matumaini Mtibwa Sugar

Makaka Mtibwa Sugar Mohamed Makaka

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga amesema kurudi kwa kipa Mohamed Makaka aliyekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuvunjika mkono wakati wa maandalizi ya msimu mpya, kumeongeza nguvu.

Mayanga anaamini makosa yatapungua eneo la ulinzi na kuepuka kuwa kapu la mabao. Mtibwa ndio inayoongoza Ligi Kuu Bara kwa kuruhusu mabao mengi katika Ligi Kuu iliyomaliza duru la kwanza ikifungwa 25 na kufunga 21 katika mechi 15 ilizocheza ikishinda sita, kupoteza tano na sare nne ikiwa na pointi 22 na imemaliza katika nafasi ya sita.

Akizungumza Mayanga alisema ana kazi kubwa ya kufanya kikosini mwake ili kuhakikisa safu yake ya ulinzi inapunguza makosa, na kuthibitisha hilo ana mpango wa kuongeza nguvu eneo hilo siku chache zijazo mara baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa.

“Makaka tangu amejiunga na Mtibwa akitokea Ruvu Shooting hajapata wakati wa kuitumikia timu kutokana na kuvunjika mkono tulipokuwa tukijiandaa na msimu mpya huu, ila sasa amerudi ameanza mazoezi, ataongeza nguvu baada ya Farouk Shikalo kuondoka,” alisema Mayanga.

“Ubora wa kipa hauwezi kuonekana kama walinzi wake hawatakuwa imara. Pia nitaongeza nguvu eneo hilo kwa mujibu wa ripoti yangu uongozi ndio utafanyia kazi ili kuhakikisha timu inamaliza ikiwa kwenye nafasi nzuri baada ya misimu miwili mfululizo kushindwa kuonyesha ubora.”

Mayanga alisema duru la kwanza la ligi hiyo lilikuwa bora na la ushindani, kwani kila timu imevuna ilichopata na kazi imebaki ngwe ya lala salama ambayo kila timu itarudi kwa ubora kutokana na maboresho ya usajili na kutetea nafasi ilizonazo kuwania ubingwa au kuepuka kushuka daraja.

Mtibwa itaanza michuano ya duru la pili kwa kuikaribisha Namungo Desemba 16 kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro kabla ya siku nne baadaye kuifuata Ruvu

Chanzo: Mwanaspoti