Kiungo Baraka Majogoro anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Chippa Utd amesema licha ya kutopata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza anaamini muda utafika.
Majogoro amejiunga na Chippa inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afika Kusini na amekaa benchi kwenye mechi mbili kati ya tatu za mwanzo hadi ya juzi (Jumamosi) dhidi ya Mamelod ndio ulikuwa mchezo wa nne na walifungwa mabao 2-0.
Akizungumza na Mwanaspoti, Majogoro amesema kitendo cha yeye kuwa kati ya wachezaji 20 katika mchezo husika, kwake ni jambo kubwa licha ya kutopata nafasi ya kucheza.
"Nafasi ipo ila inahitaji upambanaji kwa sababu hapa nimekuta watu waliokuwepo, naheshimu uwezo wao lakini nitakapopata nafasi nitapambana;
"Kweli nimekaa benchi mechi mbili na tumecheza mechi na Mamelod na nipo kwenye kikosi cha watu 20 kambini kwahiyo inaonyesha natakiwa kuwa tayari, nafasi ni suala la muda."
Akizungumzia Ligi kiujumla alisema ni nzuri na ina ushindani ambao kwa timu na wachezaji wote wanatakiwa kuwa wapambanaji vya kutosha.
Majogoro amekaa benchi kwenye mechi dhidi ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates