Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majogoro atamba kufanya makubwa

Majogoro Sauzi Baraka Gamba Majogoro

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Tuzo ya Nyota wa Mchezo (Man Of The Match) aliyopata wiki iliyopita Mtanzania, Baraka Majogoro anayeichezea Chippa United F.C kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini dhidi ya SuperSport United, imemfanya kiungo huyo kuwa na shauku ya kufanya makubwa zaidi.

Majogoro aliyeichezea KMC ya Ligi Kuu Bara kabla ya kwenda Sauzi, alisema anachotaka ni kuhakikisha kiwango chake kinaendelea kuwa bora kadiri ambavyo anaendelea kupata nafasi kwenye kikosi chake.

“Nimekuwa nikipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzangu ndio maana nimeweza kwa haraka kuendana nao na kwa pamoja kuisaidia timu kupata matokeo, kila siku nimekuwa nikipenda kuwa bora, nahitaji kucheza kwenye kiwango changu ili kuonyesha thamani yangu,” alisema.

Wiki iliyopita Majogoro alikuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya kuwapoteza viungo wa SuperSport United, Grant Margeman na Lyle Lakay kwenye mchezo huo ambao Chippa United iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Chippa United ambayo itatupa karata yake nyingine tena kwenye ligi, Jumatano kwa kucheza dhidi ya Swallows kabla ya mechi za wikiendi, ilikuwa nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 12.

Akiongelea kiwango cha Majogoro, Shadrack Mwasongwa ambaye ni mdau wa michezo nchini humo, alisema, “Anaweza kusajiliwa na klabu kubwa zaidi kama ataendelea kucheza kwenye kiwango kile, ni mchezaji mwenye mapafu ya mbwa, nilifurahia alivyocheza dhidi ya SuperSport.”

Chanzo: Mwanaspoti