Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majogoro ampasua Gadiel Michael Ligi Kuu Sauzi

Majogoro X Baraka Gamba Baraka Gamba Majogoro na Gadiel Michael

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juzi kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) iliwakutanisha Watanzania wawili, Baraka Majogoro anayeitumikia Chippa United na Gadiel Michael anayeitumikia Cape Town Spurs.

Wakali hawa wote walianza kwenye kikosi cha kwanza cha timu zao.

Baraka Majogoro akiwa na Chippa United aliondoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Town Spurs anayoichezea Gadiel. Mabao hayo yalifungwa na wachezaji Sinoxolo Kwayiba na Kayden Francis.

Kwenye msimamo wa Ligi hiyo Chippa United ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 26 katika mechi 22 ilizocheza, ikipoteza mechi 8, sare 8 na kushinda 6.

Cape Town Spurs inashika mkia, nafasi ya 16 ikivuna pointi 12 kwenye mechi 22 ilizocheza, imeshinda mechi 3, sare 3 na imepoteza mechi 16, hivyo Gadiel anaipambania timu yake isishuke daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live