Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majogoro alivyopambana na kina Mokoena wa Mamelodi

Majogoro Mc.jpeg Majogoro alivyopambana na kina Mokoena wa Mamelodi

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtanzania Baraka Gamba Majogoro ameingia Dimbani dakika ya 46 kuitetea timu yake Chippa United dhidi ya Mamelodi Sundowns juzi.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini DStv Premiership, uliopigwa katika Dimba la Lucas "Masterpieces" Moripe Stadium ulimalizika kwa Sundowns kuibuka na ushindi wa bao 2-0, mabao yakifungwa na Teboho Mokoena dakika ya 9 na Tshreeq Matthews dakika ya 85.

Teboho Makoena amefunga bao dakika ya 9 na kuwapa Uongozi Sundown. Vijana wa Chippa United walipambana kusaka bao la kusawazisha lakini haikuwa kazi nyepesi mbele ya Masandawana ambao wametoka kubeba ubingwa wa African Super League.

Katikati kulikuwa na vita ya Majogoro akiwa na Mosele wakipambana na viungo wa kiwango cha juu Bongani Zungu na Teboho Makoena.

Hivi karibuni, Majogoro aliibuka mchezaji bora wa mechi dhidi ya timu ya Richards Bay na kuibuka na ushindi wa bao 3-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: