Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majogoro akichafua Afrika Kusini

Majogoro Mc.jpeg Majogoro akichafua Afrika Kusini

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraka Gamba Majogoro amecheza dakika 79 kule DStv Premiership akiwa na uzi wa Chippa United yenye golikipa wa Nigeria, Stanley Nwabaly langoni wakati ikitoa dozi nzito Kwa Richards Bay.

Majogoro amekuwa mchezaji wa kutumainiwa ndani ya Kikosi cha Chippa United ambacho kinashika nafasi ya 10 kunako msimamo wa Ligi kikiwa na alama 23.

Majogoro alikuwa sambamba na Kamohelo Mahtlasi pale kati kukamilisha ushindi huu mnono wa Chippa United ambayo msimu uliopita chupu chupu ishuke Daraja.

Mechi nyingine Orlando Pirates imeshindwa kutamba mbele ya Cape Town City(1-1) huku Sekhukhune United ikiipa kisago Royal Am bao 1-0.

Majogoro ni Moja ya wachezaji bora eneo la kiungo pale DStv Premiership Kwa sasa atafika mbali sana huyu. Kama nchi Bado tunahitaji kuwa na kina Majogoro wengi sana. Chippa United 3-0 Richards Bay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live