Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majogoro aitwa timu ya Taifa

Majogoro Sauzi Baraka Gamba Majogoro

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo, Baraka Majogoro ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa Tanzania 'Taifa Stars' kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA dhidi ya Sudan utakaopigwa Oktoba 18 jijini Saudi Arabia.

Taarifa rasmi iliyotolewa na klabu ya Chippa United ya nchini Afrika Kusini anayoichezea nyota huyo ilieleza kuitwa timu ya taifa kwa nyota huyo licha ya kikosi kizima kinachojiandaa na mchezo huo kutowekwa wazi hadi sasa na Kocha Mkuu, Adel Amrouche.

Majogoro amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu ajiunge na miamba hiyo msimu huu akitokea Klabu ya KMC huku akikumbukwa zaidi alipotwaa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo wakati kikosi hicho kikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya SuperSport United FC.

Nyota huyo anakumbukwa zaidi mwaka 2021 katika michuano ya CHAN iliyofanyika nchini Cameroon alipofunga bao nzuri wakati timu ya taifa 'Taifa Stars' ilipotoka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Guinea kwenye mechi ya mwisho hatua ya makundi.

Bao lingine la Stars katika mchezo huo lilifungwa na beki wa kushoto, Edward Manyama na kuiacha ikimaliza nafasi ya tatu kwenye kundi 'D' na pointi nne nyuma ya vinara Guinea iliyomaliza na pointi tano sawa na Zambia zikitofautiana kwa mabao tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live