Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majirani wamwitia polisi Foden

Gfrstfdxygfdyf Phil Foden

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Majirani wa kiungo wa Manchester City, Phil Foden wamewasilisha maombi polisi ya kuwataka waende kwenye jumba la kifahari la mchezaji huyo lililopo Cheshire, Manchester kwa kile wanachodai kelele zinawabughudhi.

Gazeti la The Sun liliripoti hivi karibuni kulikuwa na sherehe ya watoto iliyofanyika hadi usiku wa manane.

Mmoja wa majirani hao alisema: "Hakuna anayejali kuhusu wao kufanya sherehe au kupiga muziki, lakini sasa imekuwa kero."

Baadhi ya majirani wa staa huyo waliliambia gazeti la The Sun, tangu Foden, mpenzi wake na watoto wao watatu wahamie, mtaa huo umekuwa kama kuzimu.

Moja kati ya mambo yanayowakera sana ni sherehe za usiku wa manane zinazowapigia kelele, pia mbwa wa staa huyo huwa wanabweka mchana kutwa.

Katika barua ya wazi, wakazi wa Prestbury, Cheshire, walimtaja Foden kama mtu mbinafsi asiyejali wenzake na wakaitaka Man City kuingilia kati.

Polisi wa Cheshire walikubali malalamiko hayo lakini wakawaambia majirani wawasiliane na manispaa kwanza.

Foden na mchumba wake wa utotoni, Foden Cooke walipata mtoto wao wa tatu wakati wa michuano ya Euro 2024, hali iliyomlazimu Foden aondoke kwenye kambi ya England kwa muda.

Chanzo: Mwanaspoti