Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Majini' yamng'ang'ania Mayele nyumbani

Mayele MsA 'Majini' yamng'ang'ania Mayele nyumbani

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya TP Mazembe imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya michuano ya CAFCL baada ya kuibamiza Pyramids FC anayoichezea Mkongomani mwenzao, Fiston Mayele.

Kwa matokeo hayo ya Kundi A, Mazembe na Mamelodi Sundowns ndiyo wamefanikiwa kutinga robo fainali huku Nouadhiboun Pyramids wakifungashiwa virago vyao mapema tu.

Mabao ya TP Mazembe yalifungwa na Joel Beya dakika ya 32, Glody Likonza dakika ya 45+1 na Patient Mwamba dakika ya 90+2 na kuwafanya vijana wa Moise Katumbi kufikisha alama 10 ambazo hazitafikiwa na timu zote mbili zilizosalia chini.

Msimamo wa Kundi A; 1. TP Mazembe - alama 10 ☑️ 2. Mamelodi - alama 10 ☑️ 3. Nouadhibou - alama 4 4. Pyramids FC - alama 4.

Majini yamng'ang'ania Mayele nyumbani kwao Congo.

Takwimu za Fiston Kalala Mayele kwenye mchezo huo. ◉ 45' — Minutes (1st half) ◉ 00 — Goals scored ◉ 00 — Assists ◉ 00 — Shot on target ◉ 00 — Aerial duels won ◉ 09 — Possession lost.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live