Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta hana uhakika kama viungo wake Thomas Partey na Emile Smith Rowe watakuwa fiti kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Everton utakaochezwa kesho.
Smith Rowe hakujumuishwa kikosini mechi mbili mfululizo Arsenal ilipocheza dhidi ya Aston Villa na Leciester City baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua.
Arsenal itaikaribisha Everton uwanja wa Emirates huku Partey akiwa hatihati, kiungo huyu aliondolewa nje ya uwanja mechi ya Arsenal ilipocheza dhidi ya Aston Villa.
Arteta huenda akamuanzisha Martin Ordegaard au Ganit Xhaka kuelekea mchezo wao dhidi ya Everton kesho uwanja wa Emirates.
Akizungumza kuhusu hali ya Partey, Arteta alisema Partey alikosa mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo kutokana na maumivu ya misuli.
"Bado sifahamu kuhusu Partey, hakufanya mazoezi lakini huenda akawepo lakini tusubiri tuone, tulimkosa katika mechi kadhaa, matumaini yangu kuona anarejea kikosini haraka," alisema Arteta.
Lakini kwa upande wa Smith Rowe huenda akaukosa mchezo wa kesho kutokana licha ya kuwekwa benchi katika mechi za ligi zilizopita dhidi ya Aston Villa na Leicester.
Kiungo huyo alikosa mechi ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City, vile vile hakujumuishwa kikosini Arsenal ilipocheza dhidi ya Brentford na Man City.
Aidha Arteta alisema anaamini wachezaji wake wanajiamini asilimia 100 baada ya kushinda ugenini michezo mitatu mfululizo.
"Tumepata ushindi mechi tatu mfululizo, hii inaonyesha vijana wanajiamini asilimia 100, sio klabu hata mashabiki wetu hawajakata tamaa, tulipoteza mechi pointi mechi tatu mfululizo, nimefurahi vijana wamerudi kwa kishindo," alisema