Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amesema anahofu na majeraha waliyoyapa wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Argentina Angel Di Maria na Paulo Dybala yanatishia nafasi zao kuelekea fainali za kombe la Dunia nchini Qatar zinazo anza Novemba 20, 2022
"Inatia wasiwasi kwa sababu ni fainali tofauti za Kombe la Dunia, zinachezwa kwenye kipindi cha tofauti na tuko karibu sana kwamba kitu chochote kidogo kinachoweza kutokea kwako kinaweza kukuacha nje. Natumai wote wawili watapona, wana muda mwingi wa kujiandaa na Kombe la Dunia. Natumai sote tunaweza kufika huko tukiwa na afya njema." Amesema Messi
Dybala alipata majeraha wikiendi iliyopita akiwa na klabu yake ya Roma na taarifa za awali iliripotiwa kuwa anaweza kukosa fainali za kombe la Dunia. kwa upande wa Mshambuliaji wa Juventus Di Maria yeye anatarajiwa kurejea uwanja mwanzoni mwa mwezi Novembe anasumbuliwa na misuli.
Kwa sasa Messi nae ana maumivu ya nyama za mguu na amekosa michezo miwili ya klabu yake ya PSG kutokana na maumivu hayo. Argentina itacheza mchezo wa kwanza wa kombe la Dunia, Novemba 22 dhidi ya Saudia Arabia mchezo wa kundi C.