Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeruhi yaendelea kumuandama Kante, kuikosa AC Milan leo

Ngolo Kanteeez Majeruhi yaendelea kumuandama Kante, kuikosa AC Milan leo

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mkabaji wa klabu ya Chelsea Ngolo Kante amekumbwa na majeraha mengine ikiwa ni siku chache baada ya kuanza kufanya mazoezi na kikosi cha timu akitokea kuuguza majeraha ya muda mrefu.

Taarifa ya Kante kukumbwa na majeraha mengine imethibitishwa na kocha mkuu wa klabu hiyo raia wa Uingereza Graham Potter huku akionesha kuumizwa na mwendelezo wa majeraha ya kiungo huyo tegemeo ndani ya klabu hiyo pamoja na timu ya Taifa ya Ufaransa.

“Kuhusu Ngolo Kante bado tunasubiri alipata changamoto mazoezini, siyo nzuri lakini inabidi tuendelee kusubiri tujue ukubwa wa hilo tatizo na tuendelee kuanzia hapo,” alisema Potter.

Kutokana na majeraha hayo mapya Ngolo Kante anakosa mchezo wa 10 msimu huu na moja ya mechi muhimu ambayo anatarajiwa kuikosa ni dhidi ya AC Milan katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA unaochezwa leo nchini Italia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live