Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeruhi waishusha presha Azam, Dabo akenua

Rdg Kocha Dabo Majeruhi waishusha presha Azam, Dabo akenua

Mon, 1 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Benchi la ufundi la Azam FC limepata habari njema ya kupona majeraha kwa nyota wanne huku likitamba kuwa wataongeza chachu katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Ofisa habari wa timu hiyo, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ aliliambia gazeti hili kuwa idadi ya majeruhi waliokuwa nao kikosini imepungua kufuatia kupona kwa nahodha Sospeter Bajana, Franklin Navarro, Daniel Amoah na Malickou Ndoye.

Zaka alisema wachezaji hao wameanza programu ya mazoezi mepesi na siku chache zijazo wataanza kufanya mazoezi ya pamoja na wenzao wa kikosi cha kwanza.

“Tuna furaha kuwajulisha wapenzi na mashabiki kuwa baadhi ya wachezaji wetu waliokuwa majeruhi wamepona na wameanza mazoezi mepesi tayari kuendelea kukitumikia kikosi chetu. Sospeter Bajana ameanza tangu Machi 28 na Franklini Navarro alishaanza hapo kabla,” alisema.

“Malickou Ndoye ameshapona na siku chache zijazo ataungana na wenzake kama ilivyo kwa Daniel Amoah. Wachezaji wengine majeruhi kama Ali Ahmada na Abdallah Kheri ‘Sebo’ wanaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa matibabu.”

Taarifa za kurejea kwa wachezaji hao zimeonekana kumkosha kocha wa Azam FC, Youssouf Dabo ambaye alisema watakuwa na msaada mkubwa kipindi hiki ambacho mbio za ubingwa zimepamba moto.

“Ni taarifa nzuri ukizingatia ligi kwa sasa ipo katika kipindi cha kuelekea mwisho na ushindani umekuwa mkubwa...kocha unahitaji kuwa na wachezaji kamili kwani mechi zinakuwa nyingi mfululizo hivyo kuna muda unafika baadhi ya wanakuwa wanachoka hivyo nafasi zao zinachukuliwa na wengine ila ukiwa na majeruhi wengi, huwezi kupata fursa kama hiyo,” alisema Dabo.

Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, imebakiza mechi tisa.

Chanzo: Mwanaspoti