Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeraha yatajwa kuichawia Chelsea

Skysports Reece James Chelsea 6245648 Majeraha yatajwa kuichawia Chelsea

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Mauricio Pochettino ametoa taarifa za majeraha ya Reece James, Robert Sanchez na Marc Cucurella baada ya Chelsea kufungwa na Everton Jumapili.

Wachezaji wote watatu walilazimika kutolewa nje wakati wa kichapo cha mabao 2-0 katika Uwanja wa Goodison Park, huku nahodha James akitolewa kipindi cha kwanza kabla ya Sanchez na Cucurella kubadilishwa dakika kumi za mwisho za mchezo.

Majeraha hayo yanaongeza kwenye orodha ndefu ya wachezaji ambao hawajaicheza The Blues.

Wesley Fofana, Romeo Lavia, Christopher Nkunku na Ben Chilwell ni miongoni mwa wachezaji wengine kumi wa kikosi cha kwanza ambao hawajacheza kwa sasa kutokana na majeraha.

“Reece alihisi kitu kwenye misuli yake ya paja. Hakika ameumia, lakini hatujui ni mbaya kiasi gani.

“Kwa kweli kwetu sisi ni mchezaji muhimu, mmoja wa mabeki bora wa pembeni duniani. Inasikitisha sana kwa sababu baada ya dakika 15 au 20 tulikuwa tunacheza vizuri na nadhani hali ya aina hii inatufanya tubadilike, kwa kweli. Malo Gusto anapata nafuu kutokana na jeraha lake.

“Hatukuwa tumetoa nafasi nyingi na unahitaji kuhamisha mambo ili kufanya mabadiliko. Hata Reece alipotoka nje timu ilikuwa ikisukuma na kucheza vizuri.

“Lakini tunasikitishwa kwa sababu unapoamini unaweza kujenga kitu na mchezaji kama yeye ambaye anafaa kuwa muhimu kwetu hawezi kuisaidia timu, tunarudi na kutathmini tena siku chache zijazo nini kinaendelea kwenye misuli yake ya paja.

Chanzo: Dar24