Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeraha yamuondoa Nchimbi Stars

Nchimbi Pic Data Majeraha yamuondoa Nchimbi Stars

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author MSHAMBULIAJI Ditram Nchimbi amekosekana katika mazoezi ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' yanayofanyika leo asubuhi katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Awali katika mazoezi ya jana Jumanne Machi 9, mchezaji huyo hakufanya kabisa mazoezi na alikuwa amekaa pembeni akiangalia wenzake.

Kocha Kim Poulsen pamoja na daktari wa timu , Richard Yomba walikuwa wakizungumza na kumuita mchezaji huyo na kuonyesha kuumia misuli ya paja.

Baada ya tukio hilo Yomba kutaka kufahamu hali ya Nchimbi alisema “Hilo litatolewa taarifa rasmi,”.

Katika mazoezi ya leo Jumatano asubuhi mchezaji huyo hajaonekana kabisa hata kuangalia mazoezi kama ilivyokuwa jana jioni.

Mtu wa karibu na mchezaji huyo kwamba, Nchimbi baada ya kuonekana hali yake inahitaji kupumzika wamemuondoa kikosini.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz