Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeraha ya Kramo yawatesa viongozi wa Simba

Kramo Majeruhi Majeraha ya Kramo yawatesa viongozi wa Simba

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba SC umesema unasononeshwa na majeruhi ya mara kwa mnara ya mshambuliaji wake Aubi Kramo ambaye aliumia tena juzi Jumamosi (Septemba 09) kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ngome FC Uwanja wa Mo Arena, Bunju.

Kwenye mchezo huo nyota huyo aliyejiunga na Simba SC msimu huu akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast alifunga moja ya mabao katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 6-0.

Hii ni mara ya tatu kwa Kramo mwenye uwezo mkubwa wa kufumania nyavu kuumia tangu amejiunga na klabu hiyo hali inayowasonesha viongozi wa timu hiyo.

Kramo aliumia wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Big Stars na kukosa mashindano yote ambapo Simba SC walitwaa ubingwa huo kwa kuwafunga watani zao Young Africans kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo huo.

Nyota huyo aliumia tena wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na kufanya aukose mchezo huo na mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Dodomna Jiji.

Akizungumza kwa njia ya simu Meneja wa Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema wao kama viongozi wanasononeshwa na kuumia mara kwa mara kwa nyota wao huyo na kuongeza kuwa leo Jumatatu (Septemba 11) wataenda kumfanyia uchunguzi wa afya yake Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.

“Kiukweli kuumia mara kwa mara kwa Kramo kama viongozi kunatuumiza sana. Ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na ameumia wakati akianza kuonyesha mchango wake kwenye timu yetu.

“Amefunga kwenye mechi zote tatu za kirafiki tulizocheza wakati huu na ni ishara ya kwamba alikuwa tayari ameanza kuimarilka na kutegemewa na timu yetu kwenye mechi za kimashindano dhidi ya Power Dynamos ya Zambia na Al Ahly katika African Super League,” amesema Ahmed Ally kwa masikitiko.

Alipoulizwa kama nyota huyo anaweza kuukosa mchezo wa Raundi ya kwanza dhidi ya Power Dynamos Jumamosi inayokuja na ule wa African Super League dhidi Al Ahly Ahmed Ally amesema, atajua hilo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake Muhimbili leo Jumatatu (Septemba 11).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: