Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeraha ya Fei Toto, madaktari wapambana

Feisal Salum Fei Toto Mayele na Fei Toto

Thu, 24 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo fundi wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, Feisal Salum 'Fei Toto' atalazimika kusubili kufanyiwa vipimo katika kambi ya timu yake, Avic Town siku ya leo Alhamisi.

Fei Toto aliumia juzi kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa katika Dimba la CCM Liti Singida Mjini nakushindwa kuendelea na mchezo huo ambao hata hivyo Yanga walishinda bao 2-0.

Imeelezwa kuwa, jopo la madaktari wa Yanga wakiongozwa na Moses Etutu pamoja na Yusup Ammar wamempatia matibabu Fei na kwa sasa anaendelea vizuri lakini watalazimika kumfanyia vipimo zaidi kabla ya mchezo dhidi ya Mbeya City, Novemba 26, 2022 kuona kama anaweza akawa sehemu ya kikosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live