Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeraha ya Curtois yanavyompa Lunin Mkataba mpya Real Madrid

Lunin Mkataba Majeraha ya Curtois yanavyompa Lunin Mkataba mpya Real Madrid

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Đorđe Petrović alipata nafasi pale Chelsea baada ya Robert Sanchez kuumia, ndio kipa namba 1 pale darajani sasa hivi.

Ayoub Lakred alipata nafasi pale Simba na anaipambania namba yake ipasavyo baada ya Aishi Manula kuumia, kazi imekuwa ngumu sana pale Simba.

Thibaut Courtois aliumia ACL kwa muda mrefu sana, amerudi kwenye mazoezi, jana amepasuka meniscus ya mguu wake wa kulia. Atakaa nje miezi miwili.

Andriy Lunin amekuwa kwenye kiwango kikubwa sana msimu huu, kwa mara nyingine tena, Lunin ataendelea kuuwasha moto kama kipa namba 1.

Hivi ndivyo nafasi huchukuliwa kwenye eneo la goalkeeping, hii ni nafasi ngumu sana kwenye mpira wa miguu. Ni jambo la kawaida sana kwa kipa namba 2 kucheza michezo miwili tu kwa msimu au hata asipate nafasi kabisa kama kipa namba 1 ni mzima wa afya, hata kama kipa namba 2 ni Bora kiasi gani.

So nafasi hizi hupatikana kwa namna hii, mwenzako akipata injury wewe itumie nafasi hiyo na performance ikiwa kubwa basi tunaanza kujihakikishia nafasi.

Real Madrid wanataka kumuongezea mkataba Lunin kwa mujibu wa Relevo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live