Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majanga ya VAR Liverpool vs Tottenham

Liver Totten Majanga ya VAR Liverpool vs Tottenham

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waamuzi wakuu walikiri kutokea kwa dosari kubwa baada ya VAR kugoma bao la kwanza lililowekwa kimiani na Luiz Diaz wa Liverpool dhidi ya Tottenham ikidaiwa kuwa ameotea.

Waamuzi hao wakuu walithibitisha kuwa makosa ya kibinadamu yamechangia makosa kujitokeza katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England kwani afisa wa VAR alisahau kumwambia mwamuzi mwenzake Simon Hopper kubadili maamuzi kwa sababu Diaz hakuotea.

Imeelezwa waamuzi waliochezesha mechi hiyo walitakiwa kurudia kwa kina ili kijidhihirisha kama kweli Diaz aliotea wakati anaingia eneo la hatari.

Gazeti la SunSport linaelewa kuwa baada ya picha za marudia kufanyika kwa kina baada ya mechi hiyo kumalizika kwa Liverpool kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspurs ilionekana wazi Diaz alikuwa sehemu sahihi.

Afisa huyo wa VAR aliyetenda makosa alitoa ishara kwamba marudio ya video yamekamilika na kuruhusu mpira kuendelea matokeo yakibaki 0-0.

Haijabainika kwa nini uamuzi huo haukuweza kutenguliwa mara tu afisa huyo ilipogundua makosa yake - badala yake akaamuru mpira kuendelea.

Taarifa ilitolewa kupitia bodi ya waamuzi ilisema; “PGMOL inakubali makosa ya kibadamu yalitokea kipindi cha kwanza katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham Hotspur. Bao la Luis Diaz lilikataliwa ikidhaniwa kuwa aliotea.

Lilikuwa kosa la wazi na bao la Diaz lilikua la halali kabisa hata hivyo, VAR ilishindwa kusaidia pia. PGMOL itapitia tena kwa ajili ya kuangalia makosa na itawasilisha kwa Liverpool."

Liverpool, ambayo ilikuwa pungufu baada ya wachezaji wao wawili kutolewa kwa kadi nyekundu ilipambana kuepuka kipigo cha kwanza msimu huu, hata hivyo dakika ya 96 Matip alijifunga na kuipa ushindi wa mabao 2-1 Spurs.

Naye kocha wa Liverpool alicharuka baada ya mechi kumalizika; "Sijawahi kuona mechi kama hii mazingira yasiyo ya haki, maamuzi ya kichaa kabisa. Kadi nyekundu ya kwanza, hata kadi ya njano ya Diogo Jota, bao la alilofunga Diaz ni halali kabisa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live