Kiungo mkabaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa N’golo Kante ameingia kwenye orodha ya mastaa ambao wako hatarini kukosa fainali za Kombe la Dunia Qatar Novemba 21 baada ya majeruhi yake kuonekana atakuwa nje kwa kipindi kirefu.
Kombe la Dunia mwaka 2022 inategemewa kuanza katikati ya mwezi ujao ambapo Kante atakuwa bado hajapona kufuatia kufanyiwa oparesheni yake.
Kante, 31, mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 2018, alipata majeruhi hayo Agosti 14 kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Tottenham ambapo mchezo ulimalizika sare ya bao 2-2.
Taarifa ya klabu imesema kuwa atakuwa nje kwa wiki nne.
Mbali na Kante, baadhi ya wachezaji wengine ambao wako kwenye hatari ya kukosa fainali hizo ni Reece James wa England, Richarlison wa Brazil, Alexander Isak wa Sweden na Diogo Jota.