Liverpool wamepata pigo kubwa la kumkosa mshambuliaji wao Darwin Nunez katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ya Liverpool dhidi ya Real Madrid siku ya Jumanne baada ya kupata jeraha la bega.
Vijana wa Jurgen Klopp walipata ushindi wa 2-0 katika uwanja wa St James’ Park na kuwashinda Newcastle United ambao wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wa EPL.
Hata hivyo, ushindi huo unaweza usisherehekewe kwa muda mrefu, huku mfungaji bao La ufunguzi Nunez akiuguza jeraha lake la bega na hivyo kupelekea wasiwasi wa kuukosa mchezo wa Jumanne UCL.
Mshambuliaji huyo wa Uruguay alitolewa nje muda mfupi kabla ya saa moja baada ya kuumia, na nafasi yake kuchukuliwa na Roberto Firmino.
Klopp aliwaambia waandishi wa habari: “Habari mbaya ni kwamba Darwin ana kitu kwenye bega lake kwa hivyo itabidi tuone.
“Ilibidi aachane na suala hilo na tunahitaji tathmini zaidi. Sijui (kiwango) kwa wakati huu ni chungu hakuna zaidi.”
Klopp atatumai kuwa Nunez atarudi tena kumenyana na wababe hao wa Hispania siku ya Jumanne, katika marudio ya fainali ya Ligi ya Mabingwa 2022.
Hata hivyo, kutokuwepo kwake kunaweza kuzibwa na Firmino au Diogo Jota.