Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majanga Liverpool, Fabinho kuikosa Fainali ya FA

Fabinho Klopp Kiungo wa Liverpool, Fabinho akitolewa nje vs Aston Villa

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha kuwa kiungo mkabaji wa kimataifa wa Brazil Fabinho atakosa mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea Jumamosi.

Fabinho aliumia kwenye mechi ya Jumanne dhidi ya Aston Villa ambapo alilazimika kutolewa nje ya uwanja na nafasi yake kuchukuliwa na Henderson, mchezo huo ulimalizika kwa Liverpool kuibutua 2-1 Villa.

Kuhusu kucheza mchezo wa mwisho wa Ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei 28, Klopp amesema kuwa mechi ya fainali kuna uwezekano mkubwa akawa sehemu ya mchezo.

Liverpool wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL nyuma ya vinara Manchester City kwa tofauti ya pointi tatu huku mechi mbili zikiwa zimesalia kumalizika kwa kandanda nchini England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live