Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majanga Liverpool, Diaz nje mechi 10, Klopp aona giza

Luis Diaz X Klopp.jpeg Luis Diaz atakaa nje mpaka mwisho wa mwezi Disemba

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Liverpool Luis Diaz imebainika kuwa atakosa michezo takribani kumi ijayo, kutokana na jeraha la goti alilolipata kwenye mchezo kati ya Arsenal dhidi ya Liverpool.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Majogoo kuendeleza na jinamizi la matokeo mabaya, baada ya kupoteza kwa jumla ya magoli 3-2, magoli ya majogoo yakifungwa na Nunez, na Firmino huku kwa upande wa Arsenal yakifungwa na Martineli, na Saka alizama kambani mara mbili na kufanya ubao usomeke 3-2 mpaka kipyenga cha mwisho

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kufikisha jumla ya alama 10 na kushika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa EPL, huku upande wa Arsenal wao wakiwa ndio vinara wa Ligi kwa alama 24 wakiwazidi Manchester City kwa alama moja.

Klopp anaendelea kukumbwa na tatizo la majeraha ambapo baadhi ya wachezaji wake tegemezi kama, Keita, Trent Alexander-Anold, Andy Robertson, Arthur Melo, Curtis Jones, na Alex Oxlade-Chamberlain

Chanzo: www.tanzaniaweb.live