Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majanga Kipa Singida Big Stars

Abubakar Khonmenyi Kipa wa Singida Big Stars, Aboubakar Khomeiny

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Singida Big Stars, Aboubakar Khomeiny huenda asirudi tena uwanjani msimu huu baada ya majeraha ya mishipa ya nyama ya kisigino.

Nyota huyo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Geita Gold aliumia akiwa mazoezini Zanzibar wakati kikosi hicho kilipokuwa kinashiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi yaliyofanyika mwezi Januari, mwaka huu.

Akizungumza na Mwanaspoti daktari wa timu hiyo, Shaaban Shija alisema kwa sasa ni vigumu mchezaji huyo kurudi uwanjani kutokana na ukubwa wa jeraha lake, hivyo ni wazi huenda akarejea pindi msimu utakapoisha na kuanza mwingine.

“Mwanzo lilionekana ni jeraha la kawaida tu, lakini kwa sasa limekuwa siriasi kidogo. Yupo Dar es Salaam kwa Dk Gilbert Kigadye ambaye ni mtaalumu wa mishipa akiendelea kumuuguza hadi atakaporudi,” alisema.

Kocha wa Singida Big Stars, Hans Van Pluijm alisema sio jambo zuri kwa mchezaji mwenye ndoto za kucheza kuonekana kukaa nje kwa muda mrefu, ingawa ni kawaida kwa wachezaji kuwatokea kutokana na kazi yao uwanjani.

“Ni mbaya kwa mchezaji na kama unavyojua nilimpendekeza asajiliwe kutokana na ubora aliouonyesha kule alikotoka nikiamini ataongeza ushindani, hivyo namuombea apone haraka na arudi katika kazi yake,” alisema.

Kuumia kwa nyota huyo kumetoa nafasi kwa Benedict Haule anayecheza mara kwa mara baada aliyekuwa kipa namba moja, Metacha Mnata kuondoka dirisha dogo la Januari na kujiunga na Yanga kwa mkopo.

Chanzo: Mwanaspoti