Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majanga Kagera: Anuary Jabir nje wiki tatu

Anuary Jabir Bh Majanga Kagera: Anuary Jabir nje wiki tatu

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa Kagera Sugar, Anuary Jabir atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu zaidi kutokana na kuchanika misuli ya paja katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Desemba 30 mwaka jana.

Anuary mwenye mabao matano hadi sasa ya TPL alishindwa kuendelea na mchezo huku akishuhudia timu yake ya zamani ikishinda mabao 2-0, katika Uwanja wa Jamhuri. Nyota huyo aliyeletwa Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi alisema itamchukua wiki mbili au tatu hadi kurejea kwake uwanjani.

“Naendelea na matibabu chini ya Daktari, Gilbert Kigadye ambaye anafanya kazi katika timu yetu ya taifa ‘Taifa Stars’, matumaini yangu ni kuona narudi uwanjani kwa wakati,” alisema Anuary.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime alisema ni pigo kubwa kumkosa mshambuliaji huyo kutokana na umuhimu wake kwenye kikosi chake licha ya washambuliaji wazuri alionao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live