Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majambazi wavamia nyumbani kwa Raheem Sterling aondoka World Cup

Majambazi Wavamia Nyumbani Kwa Raheem Sterling Aondoka World Cup Majambazi wavamia nyumbani kwa Raheem Sterling aondoka World Cup

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Raheem Sterling anaondoka katika kikosi cha cha England cha Kombe la Dunia nchini Qatar kurejea nyumbani London baada ya wavamizi wenye silaha kuivamia nyumba yake huku familia yake ikiwemo ndani yake.

Meneja wa Gareth Southgate alithibitisha taarifa hii baada ya ushindi wa England wa 3-0 dhidi ya Senegal katika timu 16 za mwisho.

"Wakati mwingine soka sio muhimu zaidi na familia inapaswa kuja mbele ," alisema Southgate.

Inafahamika kuwa tukio hilo lilitokea Jumamosi usiku. Sterling ana watoto watatu wadogo.

"Tunataka kumpatia nafasi hiyo na tutaangalia katika kipindi cha siku chache zijazo jinsi mambo yatakavyoendelea," Southgate aliongeza.

Akizungumza baada ya mechi ya Senegal mchezaji mwenzake katika kikosi cha England Declan Rice alisema:

"Nilimuona subuhi wakati wa kifungua kinywa halafu meneja akasema alikuwa na magumu nyumbani kwahiyo sote tulimtumia ujumbe."

Mechi ijayo ya England katika Kombe la Duniani ile watakayocheza dhidi ya Ufaransa katika michuano ya robo fainali siku ya Jumamosi.

Sterling ni mchezaji wa pili kuondoka katika kikosi cha England baada ya mlinzi wa Arsenal Ben White, ambaye alirudi Uingereza tarehe 30 Novemba kwa sababu zake binafsi.

Chanzo: Bbc