Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa kutoa Tuzo za Wanamichezo Bora

Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa Majaliwa Majaliwa kutoa Tuzo za Wanamichezo Bora

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Februari 10, mwaka huu kinatarajia kuzindua rasmi Tuzo za Wanamichezo Bora zinazotolewa na chama hicho.

Katibu Mkuu wa TASWA, Alfred Lucas amesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo ambao utakuwa sehemu ya tamasha la vyombo vya habari linalojulikana kama Media Day Bonanza 2024 eneo la Msasani Beach Club, Dar es Salaam.

‘’Kwa upande wa uzinduzi rasmi wa Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2024, TASWA iliunda Kamati ya Tuzo chini ya Mwenyekiti, Jemedari Said, kamati hiyo tayari imeanza kazi na imefanya uteuzi wa Mchezaji Bora wa Januari, ambaye atatangazwa siku hiyo na kupatiwa zawadi yake.

“Pia uongozi wa TASWA utatumia bonanza hilo kuzindua rasmi kamati zake ilizoteua kwa ajili ya kusaidia masuala mbalimbali ya kiutendaji, ambazo ni Kamati ya Mafunzo na Maadili chini ya Dk Egbert Mkoko, Kamati ya Fedha na Mipango inayoongozwa na CPA Shija Richard na Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu inayoongozwa na CPA Baraka Katemba.

“Nyingine ni Kamati ya Katiba inayoongozwa na Boniface Wambura, Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora iliyo chini ya Jemedari Said na Kamati ya Wanawake na Michezo inayoongozwa na Timzoo Kalugira.

“TASWA inatarajia wageni zaidi ya 2000 watashiriki bonanza na uzinduzi huo, wakiwemo viongozi kutoka vyama mbalimbali vya michezo, wanamichezo nguli wa zamani nchini na wadau wa masuala ya habari hapa nchini,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live