Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa awaangukia wadau kuchangia michezo

Majaliwa Wadau Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Waziri Kassim Majaliwa amewaomba Watanzania kuliona jambo la kuchangia timu za taifa za michezo tofauti kama wajibu wao wa msingi katika kuiletea nchi maendeleo.

Hilo amelisema leo Januari 10 wakati wa hafla ya kuzichangia timu za taifa za Tanzania za michezo tofauti ambayo inafanyika Dar es Salaam.

"Leo ni siku muhimu na ni maalum kwetu kwa sababu ni siku ya uchangiaji wa timu zetu za taifa. Ambayo tumeamua kuitisha harambee hii ambayo inahusisha wadau wa michezo na Watanzania kaa ujumla wao.

"Kiwango kinachotarajiwa kukusanywa ni Sh20 bilioni. Wakati umefika kwa Watanzania kusimama kwa miguu yetu wenyewe katika kufanya jambo letu. Michezo mingi imeweza kuonyesha kuwa Watanzania tunaweza," amesema Majaliwa.

Waziri Majaliwa amesema Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ana nia ya kuendeleza michezo na anashiriki kikamilifu katika kuipa sapoti.

"Hafla ya leo, mgeni rasmi aliyetakiwa kuwepo ni Rais Samia Suluhu Hassan lakini leo ana wageni maalum lakini anafuatilia tukio hili. Rais atazungumza na sisi muda mfupi ujao.

"Tunazo timu kwenye michezo mbalimbali ambazo zinashiriki mashindano tofauti. Mafanikio haya sio sisi ni hamasa inayoendelea kutolewa na kiongozi wetu wa nchi, Rais Samia Suluhu Hassan.

"Sasa leo hii tumeanza kuona timu nyingi zinaingia kwenye ngazi ya kimataifa na zinahitaji fedha. Michezo pamoja na mchango wake kwenye maendeleo ya taifa, michezo ni ajira lakini sasa inakwenda kusukuma na mipango yetu ya kiuchumi vilevile," amesema Waziri Majaliwa.

Chanzo: Mwanaspoti