Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maisha ya Pele katika filamu, muziki na komedi

PELE MUSIC LDK Maisha ya Pele katika filamu, muziki na komedi

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bila kujali Pele alifunga mabao 1,283 au laa katika maisha yake ya soka, waandishi wake wote wa kumbumbuku wanakubali kwamba bingwa huyo mara tatu wa Kombe la Dunia aliandika nyimbo zaidi ya 100 na aliuza nakala zaidi ya 100,000 za albamu zake.

Vile vile ameshiriki kwenye filamu kadhaa kama ile ya vita vya pili vya dunia “Victory”, filamu hizi viliwaleta watu zaidi ya milioni 3.6 kwenye kumbi za sinema nchini Brazil, huku akiwa miongoni mwa nyota wa vichekesho.

Pele aliyezaliwa Oktoba 23, 1940 jina lake kamili ni Edson Arantes do Nascimento, alifariki Alhamisi katika hospitali moja mjini Sao Paulo, Brazil akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua moyo na saratani kwa muda.

Mafanikio ya Pele kwenye uwanja wa soka yalimfanya kuwa gwiji wa michezo duniani, hata hivyo, kuna mengi na mazuri amefanya kwenye kama muigizaji na mwimbaji kama ifuatavyo;

Filamu King Pele 1962

Filamu hii inayozungumzia maisha yake iliongozwa na Carlos Hugo Christensen na kutoka rasmi mwaka 1962, ndicho kipindi ambacho Pele alishinda taji lake la pili la Kombe la Dunia nchini Chile.

Picha linaanzia katika mji wa asili wa Pele wa Tres Coracoes, inazungumza kuhusu kuhamia kwake katika jiji la mashambani la Sao Paulo la Bauru na kisha kwenda Santos ambako anakuwa nyota wa kimataifa katika soka.

Victory 1981

Hii iliyoongozwa na John Huston, ilikuwa filamu ambayo Pele alisema alifurahiya sana kuicheza maishani mwake, filamu hiyo iIlichukua mamilioni ya fedha kwenye sinema nchini Brazili.

Picha hili linahusisha wafungwa wa kivita wanaojiandaa kukabiliana na timu ya Wajerumani huko Paris, huku wakijaribu kutoroka,

Pele alicheza nafasi ya mwandishi wa habari za michezo anayeitwa Nascimento ambaye alichukua nafasi ya mlinda mlango aliyejeruhiwa wa timu inayoitwa Independencia Futebol Clube na kufunga bao la ushindi katika mechi hiyo.

Wakati huo akiwa na New York Cosmos, Pele alipata nafasi ya kucheza na wachezaji wenzake tofauti pamoja waigizaji Sylvester Stallone na Michael Caine.

Pele alisema kuwa ‘skrip’ ilitaka Stallone ndiye afunge goli la ushindi lakini mwigizaji huyo wa Marekani hakuwa na ujuzi wa kufanya hivyo, kwa hiyo aliwekwa kama kipa badala yake.

Nahodha wa zamani wa Uingereza Bobby Moore pia yuko kwenye filamu hiyo maarufu kama “Escape to Victory” inayotajwa kupata Dola28 milioni, wastani wa Sh65.3 bilioni za mauzo ya tiketi katika kumbi za sinema.

Huu ulikuwa uhusiano kati ya chapa mbili maarufu za Brazil, Pele na kikundi cha wacheshi watatu ‘Stooges’ ambao walikuwa maarufu sana kwa kipindi chao cha televisheni, Os Trapalhoes (The Clumsies).

Katika maisha yake Pele ameshiriki kwenye dokumentari kama; This is Pele (1974), Pele Eterno (2004) na Cine Pele (2011).

Televisheni

Wabrazili wanahangaikia sana michezo ya kuigiza katika televisheni kama vile wanavyohangaikia soka, Mwandishi, Ivani Ribeiro alikuwa mtu wa kwanza kumleta Pele kwenye maonyesho ya TV, Os Estranhos.

Pele aliigiza nafasi ya mwandishi maarufu ambaye aliishi kwenye kisiwa na alikuwa na marafiki zake nje ya nchi.

Mara ya mwisho Pele kuonekana katika michezo hiyo ni mwaka 2002 katika; ‘O Clone’ (Clone), alicheza mwenyewe na kuimba wimbo, Em Busca do Penta, (Seeking the Fifth). Maneno yake yalikuwa kuhusu Brazil kushinda tena Kombe la Dunia, miezi mitatu baadaye, Brazil ilishinda Kombe la Dunia kwa mara ya tano.

2. Muziki

Wimbo wake mkubwa unaitwa ‘Ginga’ ambao ulirekodiwa na kwaya na orchestra, upo kwenye albamu yake ya Samba ‘Pele Ginga’ yenye nyimbo 12 zilizoandikwa na Pele mwenyewe na ilitoka Juni 19, 2006.

Miaka mitatu baadaye, Pele alitaka kurekodi albamu nyingine kwa wasikilizaji wa kimataifa (wasioelewa kireno) na akamwalika mwimbaji wa Ireland, U2 Bono kushiriki kwenye mojawapo ya nyimbo.

Hata hivyo, mradi huo haukuweza kufanikiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa Bono alikuwa kwenye ziara za kimuziki na Band yake ya Rock, U2 iliyoanzishwa mwaka 1976 huko Dublin, Ireland.

Gwiji wa muziki Brazil, Sergio Mendez na mshindi wa Grammy (1993), mwaka 1997aliachia albamu ‘Pele’ yenye nyimbo 13 akishirikiana na Pele mwenyewe ambaye ameimba nyimbo kama; Meu Mundo É uma Bola (My World Is a Ball) na Cidade Grande (Big City).

Pia Pele aliwahi kurekodi na mwimbaji maarufu wa Brazil katika miondoko ya MPB na Jazz, Elis Regina aliyefariki Januari 19, 1982, wawili hao walitoa wimbo uitwao, Vexamao.

3. Vichekesho

Pele alikuwa mhusika katika majarida maarufu ya katuni nchini Brazili, Mchora katuni, Mauricio de Sousa na Pele ambaye alikuwa akiichezea New York Cosmos wakati huo, walifikia makubaliano mwaka 1976 kuchapishaji hadithi za watoto katika muundo wa katuni.

Hata hivyo, mwanzoni Pele hakupenda sifa za mtoto, Pelezinho, Sousa alisema katika mahojiano na vyombo vya habari.

Mchezaji huyo alitaka kuonyeshwa kama mwanamichezo mtoto mwenye nguvu, ndipo mchora katuni akatoa pendekezo kwamba awaulize watoto wake maoni yao, watoto wote wawili walipenda wazo hilo.

Sousa alitumia hadithi kadhaa kutoka utoto wa Pele katika viwanja vya Pelezinho, majarida ya vichekesho yalichapishwa mara kwa mara kuanzia mwaka 1977 hadi 1986.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live