Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mainoo kuoga minoti Old Trafford

Skysports Mainoo Kobbie Man Utd 6373626 Kinda wa Manchester United, Kobbie Mainoo

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kinda wa Manchester United, Kobbie Mainoo ataongezewa mshahara mnono baada ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Erik ten Hag msimu huu.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star, kijana huyo anakaribia kuongezwa mshahara wake wa wiki Old Trafford bila kusaini mkataba mpya.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye alijiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka tisa, kwa sasa anapokea Pauni 10,000 kwa wiki, lakini kipengele chake katika mkataba wake kinaonyesha anaweza kuongeza mshahara mkubwa.

Kiungo huyo alipewa sifa nyingi baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Everton wikiendi iliyopita akihatarisha nafasi ya Sofyan Amrabat.

Mainoo alichukua nafasi ya Amrabat alipofanyiwa mabadiliko katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Galatasaray kwenye michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya, japokuwa Mashetani Wekundu wamebana mishahara kwa wachezaji wa kikosi cha vijana, hata hivyo Mainoo anaweza kuongezewa.

Mainoo alipewa nafasi ya kuanza kwenye kikosi dhidi ya Newcastle kwenye Uwanja wa St. James Park wikiendi iliyopita, alikuwa mmoja wa wachezaji walioonyesha kiwango kizuri licha ya timu hiyo kupokea kichapo cha mabao 1-0.

Hata hivyo, alitolewa nje katika dakika ya 80 huku Ten Hag akipambana kusaka ushindi hata hivyo mashetani Wekundu walichapika.

Mainoo alisumbuliwa na majeraha kabla ya msimu mpya kuanza na alirejea kwa mara ya kwanza dimbani dhidi ya Everton mwezi uliopita ambapo United ilishinda 3-0..

Chanzo: Mwanaspoti