Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mainoo aweka rekodi tamu Euro

Kobie Mainooo Staa wa timu ya taifa ya England na Manchester United Kobbie Mainoo

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Staa wa timu ya taifa ya England na Manchester United Kobbie Mainoo ameweka rekodi bora zaidi katika michuano ya Euro 2024, akipiga pasi sahihi nyingi kuliko wachezaji wengine wa nafasi hiyo, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980.

Mainoo mwenye umri wa miaka 19, amekuwa katika kiwango bora katika michuano ya mwaka huu akicheza vyema kwenye eneo la kiungo la taifa hilo.

Kiungo huyu aliionyesha kiwango bora katika mchezo wa hatua ya 16 dhidi ya Slovakia baada ya Trent Alexander-Arnold na Conor Gallagher wote kuonekana wanafanya vibaya katika eneo hilo.

Vile vile alifanya vizuri akitokea benchi katika michezo dhidi ya Serbia na Slovenia.

Mainoo ana wastani wa kupiga pasi sahihi kwa asilimia 96.38 na amepiga pasi sahihi 133 kati ya 138 alizopiga kwenye michuano hii.

Kwa mujibu wa tovuti ya Opta, Mainoo ndiye kiungo mwenye asilimia nyingi za kupiga pasi sahihi kuwahi kutokea katika michuano ya Euro tangu mwaka 1980.

Hii inahusisha viungo ambao wamepiga pasi 100 na kuendelea na anayemfuatia katika rekodi hii ni Axel Witsel ambaye alikuwa na wastani wa asilimia 96.06 katika michuano ya Euro mwaka 2020.

Mastaa wengine walioingia kwenye 10 bora ni kama Xavi, Toni Kroos, Nigel de Jong, Vitinha na Hakan Calhanoglu.

Mainoo aliichezea England kwa mara ya kwanza mwezi Machi na alishuhudia timu hiyo ikipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Brazil.

Chanzo: Mwanaspoti