Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mainoo apandishiwa mshahara mara nne

Skysports Mainoo Kobbie Man Utd 6373626 Kobbie Mainoo

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo Kobbie Mainoo anajiandaa kupandishiwa mshahara mara nne wakati atakaposaini dili jipya la kuendelea kukipiga Manchester United, imeelezwa.

Kiungo huyo anayechipukia kwa kasi huko Ulaya, amekuwa staa mkubwa kwenye Ligi Kuu England kwa msimu uliomalizika na Man United inataka kulipa fadhila hiyo kwa kumpa mkataba safi utakaomfanya kuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa mshahara mzuri zaidi Old Trafford.

Mainoo, ambaye alifunga bao la ushindi kwenye fainali ya Kombe la FA, kwenye dili jipya atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 80,000 kwa wiki.

Kiwango hicho kitamfanya Mainoo ambaye ni staa kutokea kwenye akademia ya Man United kulipwa Pauni 5,000 kwa wiki pungufu ya kiwango anacholipwa straika wa Pauni 72 milioni, Rasmus Hojlund. Hata hivyo, bado atakuwa na safari ndefu kufikia mishahara ya mastaa Marcus Rashford, Jadon Sancho na Casemiro ambao wanalipwa zaidi ya Pauni 300,000 kwa wiki. Mainoo, 19, ameshakubaliana na dili hilo jipya, lakini kila kitu kitamalizwa baada ya Euro 2024.

Mainoo ametajwa kwenye kikosi cha awali cha kocha Gareth Southgate chenye wachezaji 33 kwa ajili ya fainali hizo za Ulaya zitakazofanyika Ujerumani baadaye mwezi huu.

Na kinda huyo ana matumaini ya kuwamo kwenye orodha ya mastaa 26 watakaounda kikosi cha Three Lions kitakachokwenda kwenye fainali hizo.

Mkataba wa sasa wa Mainoo utafika kikomo 2027 huku ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja hadi 2028. Analipwa Pauni 20,000 kwa wiki, lakini sasa dili jipya litamweka pazuri kwenye ishu ya mshahara.

Chanzo: Mwanaspoti