Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yawapa ushindi vigogo wa European Super League

UEFA SUPER LEAGUE Mahakama yawapa ushindi vigogo wa European Super League

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Haki ya Ulaya imeamua kuwa UEFA na FIFA zilichukua hatua kinyume na sheria ya mashindano kwa kuzuia kuanzishwa kwa Super League mwaka 2021.

Mahakama ya Haki ya Ulaya: "Si UEFA au FIFA inayoweza kuweka vikwazo kwa vilabu vinavyoshiriki katika mashindano mbadala."

Kwa maamuzi hayo European Super League inaweza kuanzishwa rasmi ikijumuisha vilabu 60 vyenye madaraja tofauti.

Pia Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Super League Bernd Reicart:

"Ukiritimba wa UEFA umekwisha. Soka ni bure. Vilabu sasa viko huru kutokana na tishio la vikwazo na viko huru kuamua mustakabali wao wenyewe.

"Kwa mashabiki: Tunapendekeza mechi zote za Super League zitazamwe bila malipo.l, Kwa vilabu: Mapato na matumizi yatahakikishwa kwa vilabu vyote."

Pia Kumekuwa na mawasiliano na zaidi ya vilabu 60 mwaka huu ili kuanzisha mashindano hayo.

Real Madrid na Barcelona watapokea kiasi cha €1BN kwa kuwa waanzilishi waliosalia.

Wawekezaji wengi wanataka kuingiza pesa kwenye Mashindano hayo mapya ili lianze.

NOTE: Barca na Real Madrid ndio timu pekee ambazo zilisalia baada ya kuwekewa vikwazo wakati wanataka kuanzisha mashindano haya baada ya kuwekewa vikwazo vilabu vyote vilijitoa wakabaki miamba hiyo miwili ndio maana wamepewa kipau mbele cha kupokea pesa nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live