Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yamtaka Martinez amlipe yaya wao kisa kumfuta kazi

Lautaro Martinez Mahakama Lautaro Martinez

Sun, 15 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Fowadi wa Inter Milan, Lautaro Martinez imeripotiwa kutakiwa kuilipa familia ya aliyekuwa yaya wa watoto wake kutokana na kumfukuza kazi bila kufuata utaratibu.

Kinachoelezwa ni kwamba straika Lautaro na mkewe waliamua kumwaachisha kazi mtu huyo baada ya kugundua kwamba alikuwa mgonjwa wa maradhi siriazi.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, aliachishwa kazi baada ya miezi minane ya kuwa yaya wa watoto wa Martinez, 26, huku ajira yake ilifutwa baada ya kugundulika alikuwa na tatizo la saratani.

Mwanamke huyo alifariki dunia Januari mwaka huu.

Lakini, familia yake imeibuka na kudai kwamba ndugu yao alifukuzwa kazi kinyume cha utaratibu, hivyo walimfungulia mashtaka Martinez kutokana na kitendo hicho.

Kwa mujibu wa Sport Italia, Mahakama ya Milan Jumatano iliyopita ilimtaka Martinez kuilipa fidia familia hiyo.

Hata hivyo, haikuweka wazi ni kiasi gani cha pesa Martinez alitakiwa kulipa.

Lakini, jambo hilo halijamwaacha salama Martinez raia wa Argentina na mkewe mrembo mwanamitindo wa Kiargentina, Agustina Gandolfo, kwamba hawakutendewa hadi na kuwashutumu ndugu wa mwanamke huyo kuwa wanatumia fursa.

Martinez na mrembo Agustina wamefanikiwa kupata watoto wawili, Nina, 2, na Theo aliyezaliwa Agosti.

Martinez na Agustina walijibu kwa hasira kutokana na uamuzi huo wa mahakama.

Na hapo waliamua kupeleka hasira zao huko Instagram wakiishutumu familia ya mwanamke huyo aliyekuwa yaya kwamba wanajaribu kujinufaisha.

Martinez na Agustina walidai kwamba mwanamke huyo alikuwa rafiki yao, hivyo kuna msaada mkubwa sana walikuwa wakimpatia.

Martinez amekuwa akiishia Italia tangu mwaka 2018 alipojiunga na Inter Milan akitokea Racing Club ya Argentina.

Kwenye kikosi hicho cha Inter Milan amefunga mabao 113 katika mechi 248, akishinda ubingwa wa Serie A mwaka 2021, akibeba pia Coppa Italia mara mbili na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita. Kama vile haitoshi, Martinez aliisaidia pia timu yake ya Taifa ya Argentina kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2022 huko Qatar, Desemba mwaka jana.

Chanzo: Mwanaspoti