Baada ya majadiliano ya muda mrefu klabu ya Coastal Union imefikia makubaliano ya kutoendelea na aliyekuwa nyota wa zamani wa Yanga, Juma Mahadhi kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake.
Nyota huyo aliyejiunga na timu hiyo akitokea Geita Gold ameshindwa kuonyesha makali yake, hivyo viongozi kuamua kumpa mkono wa kwa heri ikiwa ni mwendelezo wa kuachwa kwa mastaa wengi kikosini.
Taarifa za ndani zinaeleza mbali na Mahadhi ila mastaa wengine pia waliopewa mkono wa kwaheri ni William Kisinga, kipa Abubakar Abbas. Mastaa wengine ambao tayari wameachwa rasmi ni Joseph Zziwa, Emery Nimubona, Mahamoud Mroivili, Djibril Naim Olatoundji, Yema Mwamba, Yusuph Jamal na Yusuph Athuman aliyetokea Yanga kwa mkopo.