Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magwiji waitwa mezani Real Madrid

GGONFyxW4AABYu4 Toni Kroos, Luka Modric na Rais wa Madrid Florentino Perez

Tue, 14 May 2024 Chanzo: Dar24

Rais wa Mabingwa wa Soka nchini Hiapania Real Madrid, Florentino Perez, amepanga kufanya mazungumzo na viungo Toni Kroos na Luka Modric ili kuamua juu ya mustakabali wao katika wiki zijazo.

Mkataba wa Kroos na Modric unamalizika msimu huu wa majira ya joto na wanaweza kuondoka Madrid bila malipo mwishoni mwa Juni.

Wawili hao wamekuwa kwenye mikataba ya mwaka mmoja kila mmoja na ingawa walikubali kuongezewa Mei mwaka jana, Marca limeandika kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuamua juu ya kuhama kwao hadi karibu na kumalizika kwa mikataba yao ya sasa.

Madrid wamekuwa wakipanga kikosi chao kwa ajili ya msimu wa 2024/25 tangu Machi na wanatathmini soko ili kuamua kama watoe mikataba mipya kwa Kroos na Modric.

Kocha Carlo Ancelotti angependelea kuwabakiza kwa ajili ya mwendelezo, wakati viwango vyao vimethibitisha kuwa bado wana uwezo wa kucheza.

Madrid haijatoa mapendekezo yoyote makubwa kwa mchezaji yeyote katika miezi ya hivi karibuni na hivyo Perez hivi karibuni atakutana na viungo hao wawili ili kukamilisha mipango.

Kroos na Modric sio wachezaji pekee wa Madrid ambao mikataba yao inamalizika, Lucas Vazquez na nahodha wa klabu Nacho Fernandez pia mikataba yao inakaribia mwisho wa msimu huu.

Ingawa Vazquez anatarajiwa kusaini mkataba mpya na ‘Los Blancos’, Nacho ataondoka kutafuta changamoto mpya.

Amekuwa akihusishwa na klabu mbalimbali Barani Ulaya, wakiwamo mabingwa wa ltalia Inter Milan.

Chanzo: Dar24