Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magwiji waikubali Kagame Cup 2024

WhatsApp Image 2024 05 16 At 12.jpeg Magwiji waikubali Kagame Cup 2024

Thu, 16 May 2024 Chanzo: Dar24

Makocha Charles Boniface Mkwasa na Abdallah Kibadeni wamefurahishwa na uamuzi wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kurejesha michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame.

CECAFA kupitia kwa taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wake, John Auka Gecheo ilitangaza kurejesha michuano hiyo na kuitaja Tanzania Bara kama mwenyeji wake ambapo itafanyika kuanzia Julai 20 mpaka Agosti 4, mwaka huu.

Tunayo furaha kurejea kwa mashindano haya ambayo ni sehemu nzuri kwa timu zetu kujiandaa na msimu mpya na ile ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika,” alisema Gecheo.

Michuano hiyo inarejea kwa mara ya kwanza baada ya mara ya mwisho kufanyika mwaka 2021 Tanzania Bara na timu ya Express ya Uganda kushinda ubingwa huo.

Wakitoa maoni yao kuhusu kurejea kwa mashindano hayo makubwa kuliko yote katika ngazi ya klabu Afrika Mashariki na Kati, makocha wakongwe, Mkwasa na Kibadeni wote waliunga mkono uamuzi huo.

“Ni mashindano yatakayosaidia sana timu zinazoshiriki michuano mikubwa Afrika kujiandaa, itakuwa ni sawa na maandalizi yao kujiandaa na msimu mpya wa michuano mikubwa Barani Afrika na hata Ligi Kuu,” amesema Mkwasa, nahodha na Kocha wa zamani wa Young Africans.

Mkwasa ameongeza kuwa mashindano pia yatakuwa na mchango mzuri kwa Taifa Stars kupata wachezaji watakaokuwa wameimarika kutokana na kucheza mashindano hayo.

Kocha wa zamani wa Simba SC, Kibadeni pia ameunga mkono kurudishwa michuano hiyo na kusema itasaidia klabu za Young Africans, Simba SC, Azam FC na nyinginezo zitakazoshiriki michuano ya Afrika kujiandaa.

Michuano hii itajumuisha timu shiriki 16, ambapo timu 12 zitatoka miongoni mwa nchi wanachama huku nne zikitoka kwa nchi zitakazopata mwaliko.

Wanachama wa CECAFA ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudani, Eritrea, Zanzibar, Sudan Kusini, Somalia na Djibouti.

Chanzo: Dar24