Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maguri afunguka makubwa ya Zambia, Oman

Elias Maguli Elias Maguri

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wahenga hawakukosea walivyosema tembea uone na haya ndio aliyoyaona straika wa Geita Gold, Elias Maguri baada ya kucheza Zambia, Zimbabwe na Oman.

Maguri ambaye alizitumikia timu mbalimbali za hapa nchini, ikiwemo Simba kabla ya kupata ofa ya kwanza kucheza Saham Club (2015/16) na Dhofar (2016-2018), amesema kitu cha tofauti alichokiona ni thamani ya mwanamke.

"Oman ni nchi ya kidini sana, huwezi kumkuta mwanamke anatembea ovyo mtaani na hata ukimwona ana familia yake, pia kafunika kichwa, hivyo mambo ya kutongoza ovyo kule hayapo," amesema.

Alipokwenda Zambia huko alikutana na funga mwaka, kwani alipigwa butwaa siku ya kwanza kutambulishwa kwenye kambi ya timu yake mpya ya Nakambala Leopards.

"Ilikuwa jioni moja, tukiwa kambini lakini kesho yake tulikuwa tunasafiri kwenda kucheza mechi ya ugenini, sasa nikatambulishwa pale, baada ya hapo akanyanyuka nahodha kufanya maombi," amesema na kuongeza;

"Wakaanza kuimba nyimbo za kuabudu tena kwa lugha yao, walikuwa wanaimba kwa hisia kweli kweli hadi wakaanza kububujika na machozi, mara wakaanza kukemea, nikawa najiuliza kuna shida gani, baadaye nahodha akanielekeza ndio utamaduni wao kumtegemea Mungu kwa kila jambo na hata kama kuna nguvu za giza wanaamini zinaondoka kwa kuomba.

"Ibada zilikuwa zinafanyika hivi, anafungua mmoja kwa maombi, inafuatia kuabudu na sifa, anasimama mtu wa kusoma neno, likiisha yanafanyika maombi ya kumalizia, wakati mwingine alikuwa anaalikwa mchungaji kutupa neno la Mungu na anahubiri kweli kweli, yaani ni utaratibu wa timu zote za kule."

Amesema kwa upande wa Zimbabwe hawakuwa na mambo ya kusoma neno, ispokuwa kusali na kuimba nyimbo za dini tukiwa kwenye gari, "Mmoja anaanzisha nyimbo wengine tunaitikia ama kama huzijui unapiga makofi."

Chanzo: Mwanaspoti