Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magure afunguka kuhusu VAR kutumika kwenyen penalti

Harry Maguire Player Harry Maguire

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Harry Maguire anataka VAR isitumike kwenye masuala ya penalti na kadi nyekundu na badala yake matokeo yake yatumike tu kwenye masuala ya kuotea.

Klabu za Ligi Kuu England zitapiga kula kuamua kama VAR iendelee kutumika au ifutwe kwenye mkutano wa mwaka utakaofanyika mwezi ujao baada ya utata uliotokea kwenye mechi ya Wolves na hivyo kutaka kuachana na technolojia.

Beki wa kati wa Man United na England, Maguire ni mchezaji wa kwanza kuzungumzia jambo hilo kabla ya kufika siku ya kupiga kura ambayo ni Juni 6.

Maguire alisema: “Nadhani itakwenda kuwa na maoni yenye tofauti kwa sababu kuna watu wengi watataka VAR iendelee kuwapo. Lakini, kitu muhimu kwa sasa ni kuachana na teknolojia hiyo. Ilipaswa kufanya vizuri sana. Kuna sheria mpya ya kuotea inakuja msimu ujao, hapo ndipo VAR inapaswa kwenda kuwekezwa zaidi.

“Mambo yatakwenda kwa haraka sana. Binafsi nitaibakiza VAR, lakini uhusike kwenye matokeo ya kuotea tu. Ningeifuta kwenye mambo mengine yote yanayohitaji maoni. Kuotea si kitu cha maoni ni halisi.

“Ni ngumu sana kupoteza mechi kwa bao la kuotea kwa mchezaji aliyeotea kwa mita mbili au tatu. Kila mtu anafanya makosa, waamuzi wa pembeni wanafanya makosa, hiyo ndiyo sababu yangu ya kuibakiza VAR kwa ajili ya hilo tu. Lakini, nisingeitumia VAR kwenye kadi nyekundu au penalti, hiyo ingebaki kwenye uamuzi wa binadamu wenyewe asilia iwe ni ya kweli au uongo.”

Kwa muda wote msimu huu, VAR imekuwa mjadala kwenye vyumba vya kubadilishia Man United na bila shaka itakuwa hivyo kwenye klabu nyingine 19 za Ligi Kuu England.

Maguire, ambaye kwa sasa anasumbuliwa na maumivu ya kigimbi, alsiema: “Kuna mgawanyiko. Baadhi ya wachezaji wanataka ifutwe. VAR inakata mzuka sana wa kushangilia mabao. Kwa sababu kuna wakati inawafanya wachezaji washindwe kujua wanapofunga kama ni bao au sio bao. Binafsi, sipendi kuona penalti inayoamriwa na VAR - tuwaache waamuzi wa uwanjani wafanya maamuzi.

“Kumekuwa na penalti nyingi sana nyepesi msimu huu. Penalti zinaamua matokeo ya mechi, hivyo ni sehemu muhimu kwenye mechi. Mimi ni beki lazima nitasema hivyo. Mastraika wao watataka penalti nyepesi.

“Mimi sitaki kuona penalti nyepesi zinafanya timu ishinde mechi. Inapaswa iwe wazi na penalti hasa. Iwe hivyo pia kwa kadi nyekundu, waachiwe waamuzi waamue wao.

“Tunataka soka iwe mchezo wa kugusana. Tunataka soka uwe mchezo wa kutumia nguvu. Tunataka watu waende uwanjani na kutambua kwamba kuna mapambano.”

Maguire anaamini atapona kwa wakati na kuwapo kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA utakaopigwa Mei 25 dhidi ya Manchester City huko uwanjani Wembley.

Chanzo: Mwanaspoti