Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maguire ndo kama unavyosikia

Harry Maguire Player Maguire ndo kama unavyosikia

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndo hivyo, beki Harry Maguire nyakati zake za kubaki Manchester United ni kama zimefika ukingoni baada ya mipango ya mabosi wa timu hiyo, akiwamo kocha Erik ten Hag na mkurugenzi wa michezo, Dan Ashworth, kuamua jambo.

Beki huyo Mwingereza hatima ya maisha yake imekuwa na sintofahamu nyingi kwa misimu ya hivi karibuni. Alivuliwa kitambaa cha unahodha na kocha Ten Hag na ilionekana hana tena nafasi kwenye timu hiyo.

Na sasa, mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwa upande wakati katika kuelekea msimu ujao. Man United ipo kwenye mchakato wa kunasa huduma ya beki wa kati mpya kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Miamba hiyo ya Old Trafford imeshashuhudia ofa yao ya kumnasa beki wa Everton, Jarrad Branthwaite ikikataliwa, wakati beki mwingine, ambaye yupo kwenye rada zao kwa ajili ya kumsajili kwenye dirisha hili ni Matthijs de Ligt wa Bayern Munich. Na kocha Ten Hag alishaweka wazi kwamba Maguire atapoteza nafasi zaidi kwenye kikosi cha kwanza wakati Mdachi huyo atakapowasili.

Ripoti zinafichua kwamba Ten Hag ameshazungumza na Mdachi mwenzake De Ligt, kwamba anamtazama kama beki wake muhimu kwenye kikosi chake cha msimu ujao. Kocha huyo amepanga kumtumia De Ligt sambamba na Lisandro Martinez kwenye fomesheni ya 4-3-3 msimu ujao.

Jambo hilo linamfanya De Ligt ajipange kwa kulazimisha uhamisho baada ya kumalizika kwa fainali za Euro 2024 - ambapo timu yake ya Uholanzi imetinga hatua ya nusu fainali, ambapo itakipiga na England.

Wakati uhamisho huo wa De Ligt ukiwa na uhakika mkubwa wa kutokea, Maguire sasa ndiyo anakuwa kwenye wakati mgumu zaidi wa kupata nafasi, hasa ukizingatia kwamba alianzishwa kwenye mechi 18 tu za Ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live