Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maguire: msimu ujao nami nimo

Maguire Mauzo Harry Maguire

Sat, 27 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Manchester United na England, Harry Maguire amesisitiza kwamba bado yupo katika mipango ya timu kwa msimu ujao na tayari kushinda mataji akiwa Old Trafford.

Katika msimu uliopita Maguire hakupata nafasi mara kwa mara kucheza kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamwandama, jambo lililosababisha acheze mechi 22 za Ligi Kuu England na sasa amesema yupo fiti na anasubiri kwa hamu kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao. Kitasa hicho pia kimeweka wazi kuwa kmehakikishiwa nafasi katika timu, hivyo kinajiandaa kupambana.

“Labda timu iniambie kwamba nipo sokoni au sihitajiki, lakini kwa sasa vitu walivyoniambia na vitendo ambavyo timu imenionyesha nina uhakika nipo sehemu ya mipango ya timu na sasa ni muda wa kupambana na kuifanya timu ifanikiwe na kushindania mataji,” alisema

Maguire alipata jeraha la msuli mwishoni mwa msimu uliopita hali iliyomlazimu kuwa nje ya uwanja katika fainali ya Kombe la FA na pia akakosa nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya England kilichoshiriki Euro 2024.

“Ulikuwa wakati mgumu katika maisha ya soka. Nilikuwa najiandaa kwa ajili ya fainali ya FA na michuano ya Euro ili kuisaidia timu na nchi yangu,, lakini nilishindwa kucheza kutokana na majeraha.” Maguire amesafiri Man United Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na atacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal, wikiendi hii.

Chanzo: Mwanaspoti