Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maguire mambo safi West Ham, apewa kitambaa

Harry Maguire After Man Utd Concede A Goal Maguire mambo safi West Ham, apewa kitambaa

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Weat Ham United ya nchini Uingereza wamekubali ada ya uhamisho ya Pauni 30 milioni kwa ajili ya beki wa Manchester United, Harry Maguire.

Hammers ilimfukuzia beki huyo wa kimataifa wa England kipindi hiki cha usajili wa kiangazi baada ya kuvumilia unahodha.

Chelsea na Tottenham zilihusishwa na Maguire lakini West Ham ndio ilikuwa ikiongoza katika mbio za uhamisho huo.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni Sky Sports, imekubaliana masalahi ya malipo ya msimu hati hivyo dili hilo bado halijafahamika.

Sasa Wes Ham itazungumza na Maguire kwa ajili ya maslahi binafsi na atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 190,000 kwa wiki.

West Ham ilipiga hatua kubwa na kuwasilisha ombi la kuwasajili Maguire na Scott McTominay kwa Pauni 60 milioni hata hivyo ofa hiyo ikapigwa chini.

Man United ilipiga chini Pauni 30 milioni kwa ajili ya McTominay na kuiambia iongoze pesa hadi Pauni 45 milioni. Aidha lengo ilikua ni kumsajili Maguire kwa Pauni 30 milioni.

Maguire amehakikishiwa kuwa atapewa kitambaa cha unahodha West Ham kama ilivyokuwa Man United kabla kocha Ten Hag hajakinyakua na kumpa Bruno Fernandez.

Moyes bado hajafanya usajili wake wa kwanza kipindi hiki cha kiangazi na anaamini uhamisho wa Maguire utakamilika haraka iwezekanvyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: