Mlinzi wa Manchester United Harry Maguire amethibitisha kuwa hatakuwa nahodha wa klabu hiyo msimu ujao kufuatia mazungumzo na kocha juu ya mpango wa kumpatia mchezaji mwingine jukumu la unahodha wa Mashetani hao Wekundu.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Maguire ameandika ujumbe ufuatao;
“Baada ya mazungumzo na meneja leo ameniarifu anabadilisha nahodha. Alinieleza sababu zake na ingawa mimi binafsi nimekatishwa tamaa, nitaendelea kujitolea kila ninapovaa shati. Kwa hivyo nataka kusema asante sana kwa mashabiki wa Manchester United kwa sapoti yao nzuri wakati nimekuwa nikivaa kitambaa.”
“Tangu siku ilipochukua jukumu hilo, miaka mitatu na nusu iliyopita, imekuwa ni bahati kubwa kuiongoza Manchester United na mojawapo ya nyakati za kujivunia maishani mwangu hadi sasa. Ni moja ya heshima kubwa katika soka la klabu.”
“Nimefanya kila niwezalo kusaidia United kupata mafanikio - ndani na nje ya uwanja. Nitamshukuru Ole Gunnar Solskjaer kwanza kwa kunipa jukumu hilo na ninamtakia yeyote atakayechukua hatua hiyo kwa kila mafanikio na watakuwa na usaidizi wangu kamili.”