Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maguire achimba mkwara Man United

Harry Maguire After Man Utd Concede A Goal Harry Maguire

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Manchester United, Harry Maguire amefunguka kuwa ataondoka katika dirisha lijalo la majira ya baridi ikiwa hatapata nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu chini ya Kocha Erik ten Hag.

Maguire, ambaye aliondolewa kwenye nafasi ya unahodha wa Man United katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi, alipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwana cha Man United kwenye Ligi Kuu England kwa msimu huu ikiwa ni baada ya majeraha kuongezeka kwenye kikosi hicho na akaonyesha kiwango bora akifanikiwa kumtengenezea, Scott McTominay bao la pili dhidi ya Brentford.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa asilimia nyingi beki huyu kurudi benchi baada ya mabeki waliokuwa na majeraha kurudi ikiwemo Raphael Varane.

Ikiwa beki huyo ataendelea kukaa benchi kuna uwezekano mkubwa nafasi yake ya kucheza michuano ya Euro 2024 ukawa mgumu.

Maguire amesema hawezi kukaa muda wote wa mkataba wake katika kikosi hicho na akawa anacheza mara moja kwa mwezi.

“Kama haya yataendelea, nafikiri tutakaa na timu kujadili baadhi ya vitu, sio uamuzi wangu kuamua kwamba nicheze mechi ijayo au la. Nafikiri ndani ya wiki chache zijazo nitajadili hatma yangu, ninaamini kwenye uwezo wangu na ninahitaji kucheza mechi nyingi na kujihisi nina umuhimu kwenye timu,”

Kabla ya mchezo wa leo ambapo England itacheza dhidi ya Australia, Maguire alizungumza na waandishi wa habari.

“Kwa sasa sijapewa muda wa kutosha kucheza kama vile ninavyotamani, nimecheza chini ya vile nilivyohitaji,” alisema.

Katika dirisha lililopita Maguire alikuwa kwenye hatua nzuri kuondoka Man United na kutua West Ham lakini dili lilifeli katika dakika za mwisho.

“Natakiwa kuwa tayari kwa ajili ya kuchukua fursa itakayokuja mbele yangu, rekodi zangu chini ya kocha huyu (Erik Ten Hag), zinazungumza zenyewe. Asilimia za mechi ambazo timu imeshinda wakati nimecheza zipo juu, ukirudi nyuma na kuangalia mechi 15 hadi 20 za mwisho nilizocheza kwenye timu na taifa, nilifanya vizuri sana, kwa sasa nimewekeza nguvu na akili kwenye timu ya taifa lakini nitapambana pia kusalia kwenye kikosi cha kwanza nitakaporejea.”

Maguire amekuwa na wakati mgumu tangu Ten Hag apewe mikoba ya kuinoa Manchester United mwaka 2023, ameanza kwenye mechi nane tu za ligi kwa msimu uliopita na alicheza dakika mbili tu kwenye mchezo wa fainali ya Carabao ambapo Man United iliponyakua kombe hilo dhidi Newcastle.

Kwa kipindi kirefu sasa staa huyu amekuwa akikumbwa na dhihaka kutoka kwa mashabiki wa Man United ambao hawaridhishwi na kiwango chake lakini hali hiyo imekuwa haimsumbui kabisa beki huyo.

Man United inawakosa baadhi ya wachezaji kutokana na majeraha, Varane, Lisandro Martinez, Aaron Wan-Bissaka, Tyrell Malacia, Luke Shaw na Sergio Reguilon.

Chanzo: Mwanaspoti